Headlines News :
Home » » MTANZANIA RASHID ALLY KUZIPIGA NA MMALAWI WILSON MASAMBA

MTANZANIA RASHID ALLY KUZIPIGA NA MMALAWI WILSON MASAMBA

Written By Bashir Nkoromo on Friday, October 19, 2012 | 5:38 AM


Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) imetoa kibali kwa bondia Rashid Ally kupiga na Bondia Wilson Masamba wa Malawi katika Motel Paradise jijini Blantyre nchini Malawi 28th October,  2012.

Mpambano huo wa round nane katika uzito wa unjoya (featherweight) utakuwa sio wa ubingwa na utakuwa mpambano wa 50 kwa bondia Rashid Ally wakati kwa bondia Wilson Masamba utakuwa mpambano wa 24.

TPBC inamshauri bondia Rashid Ally ajiandae vizuri ili aweze kupeperusga bendera ya Tanzania vyema nchini Malawi na kuendeleza ushirikiano na urafiki wa nchi hizi mbili.

Aidha, TPBC inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu mikataba mbalimbali ya ngumi inayotiwa sahihi na mabondia wa kitanzania.

Mikataba ya ngumi duniani kote hairuhusu kutolewa kwa pesa za maandalizi au awali (advance payment) kwa mabondia wanaopambana.

Mikataba ya ngumi husainiwa kwa bondia aliyesaini kupewa pesa yake yote baada ya kushuka kwenye ulingo.

Hizi nisheria za kimataifa na mabondia wanaoendekeza tabia ya kupewa pesa za awali (advance payment) wanapotosha umma na kutia doa tasnia ya ngumi za kulipwa Tanzania.

Imetolewa na:
Uongozi, Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC)
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template