Headlines News :
Home » » BRIDGITA MISS TANZANIA 2012, AZOA SH. MILIONI NANE NA GARI JIPYAAA

BRIDGITA MISS TANZANIA 2012, AZOA SH. MILIONI NANE NA GARI JIPYAAA

Written By Bashir Nkoromo on Saturday, November 3, 2012 | 10:40 PM


DAR ES SALAAM, TANZANIA
MSICHANA Bridgit Alfred (pichani) mwenye umri wa miaka 18, kutoka Kitongoji cha Sinza 'Kwa Wajanja', Wilaya ya Kinondono mkoani Dar es Salaam,  ametwaa taji la Miss Tanzania 2012, katika shoo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Blue Pearl Hotel, uliopo ndani ya jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.

Kwa ushindi huo, kimwana huyo amezawadiwa kitita cha  Sh. Milioni 8 na gari ambalo aina yake na thamani yake vitajulikana baadaye, huku mshindi wa pili Euegene Fabian akijipatia zawadi ya Sh. Milioni 6.2 na wa tatu Eddah Sylvester sh. Milioni 4.

Washindi wengine, wa nne Milioni 3, wa tano Milioni 2.4 na wa sita hadi 15 kila mmoja akipata sh. Milioni 1.2, wakati washiriki wengine kila mmoja amefutwa jasho kwa  Sh. 700,000.

Mapema mwaka huu, Kamati hiyo iliendesha shindano dogo na kumpata Lissa Jensen ambaye aliwakilisha nchi katika fainali za Dunia kutokana na mabadiliko ya kalenda yaliyofanywa na Kamati ya Miss World na mrembo atakayetwaa taji hilo katika fainali hizo zitakazofanyika hivi karibuni atapata muda mrefu wa kufanya maandalizi.

Shindano la Miss Tanzania lilianza rasmi mwaka 1994 na Aina Maeda alikuwa mshindi wa kwanza, akifuatiwa na Shose Senare 1995, Emily Adolf 1996, Saida Kessy 1997, Basila Mwanukuzi 1998, Hoyce Temu 1999, Jacqueline Ntuyabaliwe 2000, Happiness Magese 2001, Angela Damas 2002, Sylvia Bahame 2003, Faraja Kotta 2004, Nancy Sumary 2005, Wema Sepetu 2006, Richa Adhia 2007, Nasreem Kareem 2008, Miriam Gerald 2009, Geneveive Mpangala 2010 na Salha Israel 2011.

Mapema kabla ya hapo, mwaka 1967 lilifanyika shindano la kwanza kabisa la Miss Tanzania na Theresa Shayo akashinda katika shindano lililofanyika kwenye bwawa la kuogelea la hoteli ya Kilimanjaro, lakini serikali ya Tanzania wakati huo, chini ya rais wa kwanza, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikapiga marufuku mashindano kwa sababu zilizoelezwa kwamba hayaendani na mila na desturi za Mtanzania.

Lakini Lino International Agency, ikajenga hoja ambazo ziliishawishi serikali ya Tanzania, chini ya rais wake wa pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuruhusu mashindano hayo yafanyike tena, ingawa mwaka 2001 yaliponea chupuchupu kufutwa tena, enzi za rais wa awamu wa tatu, Benjamin William Mkapa.
Ilitokana na vazi la kuogelea ‘kichupi’, ambalo lilipingwa kwa sababu linamdhalilisha mwanamke wa Tanzania, lakini Lino ikaboresha kipengele cha vazi hilo, kutoka la kuogelea hadi la ufukweni, ambalo kidogo linamsitiri binti na serikali ikaruhusu mashindano yaendelee.

Hata hivyo, mabinti wanapokwenda kwenye shindano la dunia, wanavaa vazi la kuogelea kupanda jukwaani, katika shindano ambalo linaonyeshwa moja kwa moja nchi zaidi ya 100 duniani na picha zao kuchapishwa kwenye majarida, magazeti na mitandao mbalimbali duniani.

Bridgit sasa atashiriki shindano la Miss World mwakani, baada ya Lisa kushiriki mwaka huu na kuanzia sasa atakuwa akiandaliwa kwa ajili ya fainali hizo. 
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template