Headlines News :
Home » » LINA NA BARNABA KUTUPIWA VILAGO THT? KISA SHOO YA LADY JAY DEE.

LINA NA BARNABA KUTUPIWA VILAGO THT? KISA SHOO YA LADY JAY DEE.

Written By Bashir Nkoromo on Thursday, May 16, 2013 | 9:51 AM

LADY JAY DEE

DAR ES SALAAM, Tanzania
Wakati shoo maalumu ya Miaka 13, ya mwanamuziki nguli wa bongo fleva nchini na kiongozi wa bendi yenye msisimko mkubwa ya ‘Machozi Band’, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ au Jide’ ikizidi kunukia, huenda kwa upande wa wasanii wa Nyumba ya Vipaji ya THT, Linah Sanga na Barnaba  mwaka huu ukawa mchungu kwao kufuatia kuwepo taarifa za kutimuliwa na uongozi wa juu.

Vyanzo kutoka kwa mtu wa karibu wa Linah vimeeleza kuwa mpaka sasa msanii huyo hana raha na wala hajui ataanza vipi katika harakati zake za kimuziki hasa kufuatia hivi karibuni kukacha shoo ya nguli Lady Jay Dee kwa shinikizo kutoka kwa wakubwa zake wa kazi.

Inadaiwa uongozi wa juu wa Linah umekaa kikao na hatua iliyofuatia kwenye kikao hicho ni kuwaondoa kabisa THT na Barnaba kwa tuhuma kwamba huenda wakatia doa wasanii wenzao ndani ya kundi hilo.

“Juzi Lina, haikuwa kawaida yake maana hata alipopigiwa simu na mtu mmoja kwa ajili ya hatua zingine alionekana kuw na hofu, na wala hakutaka kusikia ushahuri wangu ambao nilikuwa nikimhusia kuwa aachane na mawazo hayo kwani jambo analoliwaza huenda likaisha na hata maamuzi yatakayotoka yatakuwa ni kawaida” kilieleza chanzo kutoka kwa mtu wakaribu wa Lina, amabaye hata hivyo alisema kuwa huenda ukweli wa jambo ukawa hadharani.

Taarifa za ndani za uongozi wa THT zilibainisha kuwa mpango wao wa kuwashughulikia wasanii hao upo pale pale na taratibu zinafuata ili zisilete madhara kwa wasanii waliopo ndani ya THT  na watu wa karibu wanaoiunga mkono THT.

“Wewe nani kakwambia kama tumewaadhibu Lina na Barnaba?, ndio kwanza tunakusikia wewe hizo taarifa,  sisi tunafanya mambo yetu wao waache wafanye yao tukiwa nao sie na tunaouwezo wa kuwatimua ili kulinda hadhi ya THT” Kilieleza chanzo hicho ambacho hata hivyo kutokana na usalama wa jina lake tumelihifadhi.

Aidha, katika ‘ku-balance’ uhondo kamili wa habari hizi wasanii hao wote walipotafutwa kwenye simu zao za mkononi hawakuweza kuwa hewani kwa muda mrefu.. na hata alipopigiwa mtu wao mmoja wa karibu naye alizima simu.

Katika kile kinachoeleza kupamba moto shoo hiyo ya Jide, na kujaa kwa taarifa mbalimbali juu ya wasanii watakaopamba shoo ya miaka 13, Mei 31 ndani ya Nyumbani Lounge, Tayari tiketi zimeanza kuuzwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Saalam.

Inaelezwa kwamba katika shoo hiyo ya kijanja ndani ya Nyumbani Lounge, patakuwa hapatoshi pale wadau wa burudani na wastaarabu wote watakapojumuika kwa pamoja ku-shoo love kwa Lady Jay Dee  na Machozi Band, huku listi ya mastaa mbalimbali wanatarajia kuhudhuria sambamba na ‘surprise’ kutoka kwa mastaa hao ambao kwa sasa wengi wapo kimya wakihofia kutengwa na wazee wa ‘fitina bin Logiki’.

Awali kulikuwapo na taarifa za kuwapo kwa msanii Matonya, ambaye mtandao wa Lady Jay Dee ulitoa hadharani kuwa mwanamuziki huyo ameshachukua ‘advance’ ingawa inaelezwa kwamba naye ameshamtishwaili ajitoe, lakini akiwa ameshatafuna pesa ya watu.

Mtandao huo wa Jide umenukuu kila kitu juu ya Makubaliano baina ya Capt.Gadna G Habashi na Matonya ambapo pia unaweza kuyasoma kupitia (Ladyjaydee.blogspot.com) Pia ulitoa kwa mara ya kwanza picha,maelezo muhimu na video ya wanamuziki hao wawili Linah na Barnaba wakiingia mkataba wa shoo hiyo na pia kuhamasisha watu kufika Mei 13.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template