1

2

3

4

5

Friday, April 18, 2014

MPIGA GITA SKYLIGHT BAND AFARIKI DUNIA

 10173726_10152036323227864_1413106576404088176_n
Mpiga Gitaa wa Skylight Band maarufu kwa jina la Chiri Challa(pichani) amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia April 17 katika Hospitali ya Muhimbili.
Taarifa za awali zimethibitishwa na uogonzi wa bendi hiyo kuwa mpiga gitaa huyo machachari amefariki baada ya kuugua kwa siku mbili ugonjwa wa kupooza nusu ya mwili wake na kuepelekea kutofanya kazi ipasavyo.
Kwa mujibu wa Meneja wa bendi hiyo Aneth Kushaba AK47 Ugonjwa wa kupooza ulipelekea mishipa ya damu kichwani kupasuka hivyo na kumsababishia maumivu makali sehemu kichwani.
10268531_10152035773597864_7736400417218686840_n
Kutokana na msiba huo uongozi unapenda kutoa taarifa kuwa Show ya Escape One iliyokuwa ifanyike Alhamis ya April 17 imeahirishwa hata hivyo uongozi unasikitika kumpoteza msanii huyo ambaye alikuwa ni kiungo muhimu wa bendi na inaungana na familia ya marehemu Chiri Challa kuomboleza kifo cha mpendwa wao na inatoa pole kwa familia na mashabiki wa Skylight Band na wapo bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu.
Msiba na shughuli za mazishi zinafanyika maeneo ya Mwanyamala Ujiji mtaa wa Mpunga.
Kwa mawasiliano zaidi namba ya Meneja wa Bendi +255 715 677 499.

Friday, April 11, 2014

MIYEYUSHO,CHEKA,KING CLASS MAWE WAPIMA UZITO KUPAMBANA LEO

Bondia Mustafa Dotto kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'KIng class Mawe' kabla ya kuzipiga katika ukumbi wa PTA Sabasaba April 12 siku ya jumamosi katikati ni Promota Jay Msangi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Mustafa Doto utakaofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Sukkasem Kietyongyuth kushoto akiwa na kocha wake Win Panyaparichot wakati wa upimaji uzito
Bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika PTA Sabasaba April 12 siku ya jumamosi picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
 Bondia Fransic Cheka akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa kesho April 12 katika ukumbi wa PTA Sabasaba kushoto ni bondia Gavad Zohrehvand wa Iran picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Baadhi ya waandisi wa habari wakishuhudia wakati mabondia hao wakipima uzito

Friday, April 4, 2014

TSN BOYS KUKABILI MWANANCHI MEDIA KOMBE LA NSSF: MROKI AIAHIDI DAU NONO


Kikosi cha TSN Boys
TIMU ya soka ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inashuka dimba la Sigara, Chang’ombe, Dar es Salaam kuikabili Mwananchi katika Kombe la NSSF kwa Vyombo vya Habari 2014.

Mechi hiyo itakayochezwa saa 2 asubuhi, itakuwa muhimu kwa timu zote mbili kwani mshindi atasonga mbele katika hatua ya robo fainali zitakazoanza Jumatatu ijayo.

TSN imetinga hatua hiyo baada ya kupewa ushindi kutokana na wapinzani wao, Mlimani Media kuwatumia wachezaji ambao hawakuwa halali. Mlimani Media ilikuwa imeshinda kwa mabao 9-0.

Mwananchi ni mechi yake ya kwanza. Mbali ya mechi hiyo, mechi nyingine kesho ni kati ya Tumaini dhidi ya Sahara Media, wakati upande wa netiboli, itakuwa ni mechi za robo fainali kati ya Business Times dhidi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), wenyeji NSSF dhidi ya Tumaini Media.


TSN Boys wapo katika hamasa na ari kubwa ya mchezo huo wa kesho ambapo Meneja wa Timu hiyo, Mroki Mroki "Father Kidevu"  ameahidi kuzawadia mfungaji wa kila goli kitita cha shilingi 5,000. "Niliahidi katika mchezo wa awali na hata sasa bado ahadi yangu ipo pale pale kwa kila goli nitalilipia shilingi 5,000 nahiyo haina longolongo lengo ni kuhamasisha ushindi kwa timu yetu," alisema Mroki.Aidha Mroki amesema atakuwepo uwanjani kuhakikisha ushindi unapatikana kwa vijana wa TSN Boys na kusonga mbele katika mashindano hayo. 


Katika mechi za jana, mabingwa watetezi wa soka, Jambo Leo walitolewa baada ya kufungwa mabao 2-1 na Free Media kwa mabao ya Saleh Mohammed.

Bao la Jambo Leo lilifungwa na Zahoro Mlanzi. Aidha, Changomoto ilisonga mbele baada ya kuilaza New Habari kwa penalti 7-6, baada ya sare ya bao 1-1. Free Media na New Habari zilisonga mbele kama timu bora mbili zilizoshindwa, lakini zikiwa na matokeo mazuri (best looser).

Katika netiboli, Mlimani Media ilishindwa kutamba kwa Habari Zanzibar kwa kufungwa mabao 19-15, wakati IPP iliizamisha Global Publishers kwa
mabao 27-8.

Saturday, March 29, 2014

LADY GAGA AFANYA VITUKO VYA MWAKA KWENYE BETHIDEI YAKE


Lady Gaga 1

Mwanamuziki wa pop asiyehishiwa  vituko kila kukicha, Lady gaga ametoa mpya baada ya kuvaa nguo iliyomuacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake kiasi kwamba unaweza ukaona kila kitu alichovaa kwa ndani wakati  akisherehekea  siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 28  iliyofanyika katika ukumbi wa ‘Roseland Ballroom’ New York Marekani 

”Asanteni sana kwa kujumuika na mimi kwenye bethidei yangu, nilipoamka asubuhi nilikuwa na furaha. Nilikuwa nahamu ya kuwepo hapa usiku huu. Nina marafiki wengi hapa..mashabiki wengi na nimekulia kwa miaka sita” alisema Gaga
Lady GagaLady Gaga

LULU COVERS VIBE TZ MAGAZINE APRIL 2014 ISSUE


Lulu on vibe

Lulu1

Friday, March 21, 2014

MAANDALIZI TAMASHA LA PASAKA YAKAMILIKA

MKurugenzi wa Msama Promotions Ltd,ambao ndio waandaji wa tamasha la krismass na Pasaka,Bwa.Alex Msama amesema kuwa maandalizi ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kuanza kufanyika jijini Dar mnamo April,20 mwaka huu yamekamilika.

Aakizungumza na Waandishi wa habari jijini dar leo katika viwanja vya Karimjee,Msama amebainisha kuwa kila kitu kimekwishakamilika,wakiwemo wasanii mbalimbali watakaotumbuiza siku hiyo,aidha amesema kuwa pamoja na wanamuziki wa nyumbani kushiriki tamasha hilo,pia kutakuwepo na wanamuziki wengine kutoka nje ya nchi.

Msama amesema kuwa katika kuhakikisha washabiki na watazamaji wanalifurahia tamasha hilo lenye kujaa nyimbo za kumsifu na kumuabudu Mungu,kutakuwepo na wanamuziki nyota kutoka nchini Afrika kusini,ambao watalipamba vyema tamasha hilo.

"Katika tamasha hilo kutakuwepo na wanamuziki kutoka Afrika kusini,akiwemo Rebecca Malope  mbaye atatumbuiza kwenye hitimisho la tamasha hilo jijini Mwanza,pamoja na Mwanamuziki Kekeletso Phoofolo ambaye atatumbuiza hapa jijini Dar,wakiwemo na wanamuziki wengine wengi wa hapa nyumbani kama vile Rose Muhando,Upendo Nkone,Bon Mwaitege,John Lisssu,Upendo Kilahilo na wengineo wengi" alisema Msama.
Msama amesema kuwa Tamasha hilo litazunguka mikoa isiyopungua tisa,ameongeza kuwa pia katika kuisadia jamii,Kamati ya maandalizi ya tamasha la pasaka itaandaa fungu Maalum kwa ajili ya kuwapa Mayatima na watoto waishio katika mazingira magumu.

Sisi kama Msama Promotions tutaandaa fungu rasmi kwa ajili ya kusaidia watoto Yatima,lengo likiwa ni kuwapa fungu maalum kwa ajili ya kujitegemea,mfano kuwaanzishia biashara ambayo itakuwa endelevu na yenye kuwasaidia badala ya kupewa vitu vya kupita tu kila wakati"alisema Msama.

Amesema kuwa watatoa fungu maalum kwa kila kituo kwa kuwapa kiasi cha shilingi Milioni tano kwa kila kituo ili kujiendeleza zaidi,na tunalitoa kutokana na mapato ya Pasaka,na mapato mengine yatatumika kuendeleza ujenzi wa kituo cha watoto waishio katika mazingira magumu ,Kituo cha Watoto kiitwacho Jakaya Mrisho Kikwete rafiki wa wasiojiweza.

Wednesday, March 19, 2014

TASWA YATAZAMA TUZO ZA WANAMICHEZO BORA

KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) iliyokutana jijini Dar es Salaam wiki iliyopita ilikubaliana kufanya mabadiliko makubwa katika Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania zinazotolewa kila mwaka na TASWA.
 
Kikao kilijiridhisha kuwa tuzo za TASWA zina heshima kubwa na wanamichezo hapa nchini wanazithamini na kuzitegemea kuliko tuzo za aina nyingine zozote.
 
Lakini kikao kilikubaliana kuwa pamoja na hayo bado kuna changamoto mbalimbali kuhusiana na tuzo hizo, hivyo kuna haja ya kuhakikisha zinaboreshwa zaidi ya ilivyo sasa.
 
Kutokana na hali hiyo, kikao kiliunda Kamati Maalum ya watu 12 Kusimamia Tuzo hizo, ambayo itakuwa chini ya uenyekiti wa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TASWA, Rehure Nyaulawa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio 100.5 Times FM na ina wajumbe wengine 10 ambao si viongozi wa TASWA, lakini ni waandishi wazoefu wa habari za michezo, hivyo tunaamini wataleta ufanisi.
 
Jukumu la kamati hiyo pamoja na kuandaa mchakato wa upatikanaji wa Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2013 na kupanga tarehe ya kufanyika tuzo hiyo mwaka huu, lakini pia imepewa mamlaka ya kutazama mfumo wa tuzo ulivyo na ikiwezekana kuubadili kwa namna itakavyoona inafaa kwa maslahi ya chama na maendeleo ya michezo kwa ujumla.
 
Ni nia ya Kamati ya Utendaji ya TASWA kuona tuzo inakuwa bora na ambayo wadau wa michezo wataendelea kuiheshimu kwa kila hatua. Hivyo kuamua kuipa kamati hiyo mamlaka ya kuamua mambo ya msingi katika kuiboresha kwa mipango ya muda mfupi na mrefu.
 
Licha ya Mwenyekiti Nyaulawa, wengine walioteuliwa kuunda kamati hiyo na vyombo vyao katika mabano ni Elizabeth Mayemba (Mwandishi wa Majira), Amour Hassan (Mhariri wa habari za Michezo-Nipashe), Dominick Isiji (Mhariri wa michezo-The African) na Rais wa Chama cha Gofu Wanawake Tanzania (TLGU), ambaye pia ni mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Daily News, Mbonile Burton.
 
Wengine ni Mahmoud Zubeiyr (mmiliki bongostazblogspot), Athanas Kazige (Mwandishi Uhuru), Suleiman Jongo (Mwandishi-Citizens), Angela Msangi (Mwandishi TBC1) na Cosmas Mlekani (Mwandishi-Spotileo) na Tulo Chambo ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Riadha Tanzania (RT) na pia Mhariri wa habari za michezo wa gazeti la Tanzania Daima.
 
Katibu wa kamati hiyo atakuwa Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando na kikao cha kwanza cha kamati kitafanyika jijini Dar es Salaam Jumatatu Machi 24, ambapo kitafunguliwa na Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto, ambaye kwa sasa yupo safarini.
Ahsanteni.
 
Egbert Mkoko
Kaimu Mwenyekiti TASWA
19/03/2014
 
0759-773727