Headlines News :
Home » » TAARIFA KUTOKA TASWA

TAARIFA KUTOKA TASWA

Written By Bashir Nkoromo on Wednesday, May 7, 2014 | 4:34 AM

 A; MKUTANO MKUU AIPS
 
WIKI iliyopita kulifanyika Mkutano Mkuu wa Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS) jijini Baku, Azerbaijan.
 
Mkutano huo ulishirikisha viongozi wa vyama 116 vya waandishi wa habari za michezo duniani, ambapo Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kiliwakilishwa na Katibu Mkuu, Amir Mhando.
 
Katika mkutano huo msisitizo mkubwa umewekwa kwa nchi wanachama kutilia mkazo program za kuwaendeleza waandishi chipukizi wa habari za michezo, lakini pia AIPS yenyewe nayo pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Afrika (AIPS-Afrika) vimechukua jukumu la kusaidia kwa wale watakaokidhi vigezo wanavyohitaji.
 
Hivyo kila nchi mwanachama itatuma wasifu wa majina ya wanahabari chipukizi wasiozidi watano, ambao AIPS yenyewe itaangalia wale watakaofaa na kuwaandalia mafunzo baadaye mwaka huu.
 
Kwa upande wa AIPS Afrika yenyewe itaendesha mafunzo kwa wanahabari chipukizi 25, ambayo yatafanyika Morocco, lakini kipaumbele cha kwanza kitakuwa kwa nchi 16 zitakazocheza fainali za mataifa ya Afrika mwakani nchini humo na nafasi zingine zitabaki kwa nchi ambazo hazitaenda Morocco.
 
Mafunzo ni ya wazi kwa waandishi wowote chipukizi wasiozidi umri wa miaka 25, hata wale waliopo kwenye vyuo vya uandishi wa habari wataruhusiwa kuomba. Tanzania imewahi kupata nafasi moja mwaka 2011, ambapo Mwita Mwaikenda wakati huo akiwa mwanafunzo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alishiriki mafunzo hayo yaliyoandaliwa na AIPS akiwa miongoni mwa Waafrika watatu tu waliopata nafasi hiyo.
 
Utaratibu kuhusiana na suala hili utaelezwa vizuri baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya TASWA kitakachofanyika Jumatatu wiki ijayo kujadili masuala mbalimbali.
 
 
B: Ziara Uganda
Kulifanyika kikao cha viongozi wa nchi wanachama wa AIPS ambao wanatoka Afrika Mashariki, ambapo nchi za Burundi, Kenya, Tanzania na Uganda zilishiriki na kukubaliana kufanyike ziara ya kimafunzo itakayohusisha waaandishi wa habari za michezo Septemba 25-29 mwaka huu Kampala, Uganda. Rwanda licha ya kutoshiriki mkutano wa AIPS, lakini tulikubaliana nayo ialikwe.
 
Katika makubaliano hayo kila nchi itakuwa na washiriki wasiopungua 20 na wasiozidi 35, ambapo pia litafanyika kongamano kuhusiana na masuala mbalimbali ya waandishi wa habari za michezo kwa ukanda huo na siku ya mwisho litafanyika bonanza la michezo mbalimbali. Taarifa zaidi za ziara hiyo itatolewa siku za usoni.
 
C; Ushirikiano wa kimafunzo
 Baadhi ya nchi zilizoshiriki mkutano huo wa 77 wa AIPS, zilikubaliana kuanzisha utaratibu wa kubadilishana utaalamu wa kitaaluma kwa nchi mbalimbali, kwa kuwatoa baadhi ya wanahabari kwenda nchi zilizo katika makubaliano hayo kujifunza kwa gharama za nchi mwenyeji.
 
Hata hivyo makubaliano hayo, yataanza kufanya kazi baada ya kila nchi kupata baraka za Kamati ya Utendaji na kutuma majibu kwa waratibu kwamba wanaafiki. Kamati ya Utendaji ya TASWA katika kikao chake kijacho hilo litakuwa moja ya ajenda.
 
Nawasilisha.
 
Katibu Mkuu TASWA
07/05/2014
 
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Total Pageviews

Comments

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. theNkoromo SPORTS - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template